Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika


Utangulizi
Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika ilianzishwa mwaka 1987 wakati Idara ya Isimu na Lugha za Kiafrika ilipogawanywa kuwa Idara tatu ambazo ni: Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Idara ya Lugha za Kigeni na Idara ya Kiingereza.

Mahali Ilipo
Idara hii ipo kwenye Barabara ya Makongamano (Conference Road), karibu na Idara ya Fasihi na Idara ya Kiingereza na Isimu, ikiwa nyuma ya Kituo cha Biashara na mkabala na mkabala na kanisa dogo la chuo kikuu.

Wahadhiri na Maeneo yao ya Utaalamu
Idara hii inao wahadhiri ishirini na wanne (24) katika mabewa tofauti ya chuo hiki (Bewa Kuu, Kitui, Ruiru, Mombasa, Migori, Nyeri, Nakuru na Kericho).  Maeneo ya utaalamu ya wahadhiri hawa ni pamoja na:
 • Historia na Maendeleo ya Kiswahili
 • Mofolojia
 • Isimujamii
 • Sintaksia
 • Fasihi Simulizi
 • Toni katika Lugha za Kibantu
 • Maswala ya Jinsia katika Fasihi
 • Mbinu za Mawasiliano
 • Maswala ya Ulemavu katika Fasihi
 • Ushairi wa Kiswahili
 • Fasihi ya Watoto
 • Mabadiliko katika Lugha
 • Fasihi ya Kiafrika
 • Tafsiri ya Ukalimani
 • Fasihi Linganishi
 • Sanaa za Maigizo
 • Nadharia za Uchanganuzi wa Fasihi
 • Sarufi ya Kiswahili
 • Fonolojia
 

Upekee wa Idara Hii
Idara hii inatambulika kwa ukubwa wake tukizingatia idadi ya wanafunzi na ubora wa kozi zinazofundishwa.

Shahada ya Kwanza
Idara hii hufundisha wanafunzi wa shahada za B.A. na B.ED.  Wanafunzi hawa hutathminiwa kupitia kwa kazi ya darasani na mitihani.

Shahada ya Uzamili
Masomo ya Shahada ya Uzamili ya Kiswahili hudumu miaka miwili: ikiwa ni mihula mitatu ya kazi za darasani na muhula mmoja wa kuandika tasnifu au mihula miwili ya kazi za darasani na mihula miwili ya kuandika tasnifu.  Sasa hivi Idara ina zaidi ya wanafunzi 200 wa Shahada ya Uzamili.

Shahada  ya Uzamifu
Shahada ya Uzamifu katika Idara hii hutolewa kupitia kwa uandishi wa tasnifu.  Hivi karibuni, masomo ya darasani kwa ajili ya shahada hii yataanzishwa.  Mwanafunzi anaruhusiwa hadi miaka mitatu kukamilisha shahada hii.  Kuna zaidi ya wanafunzi kumi wa Shahada ya Uzamifu waliojisajili Idarani.

Nyenzo
Idara ina maktaba ndogo ambamo mnahifadhiwa vitabu, majarida na tasnifu za Kiswahili.  Tunawawezesha wanafunzi kutumia maabara ya lugha ya chuo katika tafiti zao za kiisimu.

Mfumo wa Masomo
Kuna mifumo mitatu ya masomo: (a) mfumo wa muda wote (b) mfumo wa masomo ya likizo (c) mfumo wa masomo huria.  Mwanafunzi huchagua mfumo anaopendelea.

Kazi
Baada ya kufuzu, wanafunzi huajiriwa kama walimu, wahariri, watafiti, watawala, wanahabari, wafasiri, wakalimani au hata wanaweza kujiajiri.

Last Updated on Wednesday, 01 March 2017 14:39